Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 31
Atletico Madrid v Real Mallorca
Estádio Cívitas Metropolitano
Madrid, Spain
Wednesday, 26 April 2023
Kick-off is at 20h30
Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Real Mallorca kwenye
mechi ya La Liga ugani Estádio Cívitas Metropolitano Aprili 26.
Matokeo ya hivi karibuni
Atletico, maarufu kama the Mattress walipoteza 1-0 dhidi ya FC Barcelona ugenini Aprili 23 na kufikisha kikomo msururu wa mechi 13 bila kupoteza katika ligi.
Hata hivyo, Atletico hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi 7 za ligi zilizopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi wa mechi sita na kupata sare moja ugani Estádio Cívitas Metropolitano.
Mallorca waliibuka na ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Getafe CF Aprili 23, ikiwa ni mechi yao ya nne mfululizo kwenye ligi bila kupoteza.
Vile vile, The Pirates hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo miwili iliyopita wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare moja na kushinda mechi moja.
Athari ya matokeo ya mechi hii
Atletico wanashikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la ligi na wanatarajia kumaliza nne bora ifikapo mwisho wa msimu.
Chini ya Diego Simeone, Atletico wanatarajia kupata ushindi dhidi ya Mallorca ambao wanazidi kuonyesha mchezo mzuri na kupata matokeo mazuri hadi msimu huu.
Mallorca wapo katika nafasi ya 10 na ushindi dhidi ya Atletico utawapa fursa kubwa ya kumaliza ligi katika nusu ya kwanza ya jedwali.
Vikosi
Atletico hawana mchezaji anayetumikia marufuku au adhabu ila wanauguza mejeraha ya wachezaji Memphis Depay na Reinildo Mandava watakaokosa mechi hiyo
Mallorca hawana majeruhi yeyote. Pablo Maffeo na Antonio Sánchez wapo hatarini ya kutumikia marufuku ya mechi iwapo wataonyeshwa kadi ya njano.
Wachezaji muhimu
Alvaro Morata ndiye mfungaji bora wa Atletico akiwa na magoli 10 msimu huu. Mshambuliaji huyo wa Uhispania anatarajiwa kuongoza timu hiyo kupata ushindi dhidi ya Mallorca.
Kwa upande mwingine, Mallorca wataweka matumaini yao kwa mchezaji Vedat Muriqi ambaye amefanikiwa kufunga magoli 12 na kusaidia kupatikana kwa magoli mawili msimu huu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nukuu
“Hatukushambulia vya kutosha,” alisema Simeone baada ya kushindwa na Barcelona.
"Aintone Griezmann alikosa nafasi nzuri sana ya kufunga bao na kasha tukaadhibiwa na goli zuri la mchezaji Ferran Torres.
“Umakini katika mechi kama hizi ndio unakupa ubingwa. Ukishambulia vizuri na kuchukua nafasi zako katika eneo la mpinzani ni rahisi kupata ubingwa.”
Matokeo baina ya timu hizi
Mallorca waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico katika mechi ya mwisho ya ligi baina yao ugani Estadi Mallorca Son Moix Novemba 9 2022.
The Pirates hawajapoteza mechi yoyote katika mechi tatu za mwisho za ligi dhidi ya Atletico huku wakiandikisha ushindi mara tatu mfululizo.
Ratiba ya mechi za La liga, mchezo wa 31.
Aprili 25 Jumanne
8:30pm - Cadiz CF v CA Osasuna
8:30pm - Girona FC v Real Madrid
11:00pm - Real Betis v Real Sociedad
Aprili 26 Jumatano
8:30pm - Atletico Madrid v Real Mallorca
8:30pm - Getafe CF v UD Almeria
11:00pm - Celta Vigo v Elche CF
11:00pm - Rayo Vallecano v FC Barcelona
Aprili 27 Alhamisi
8:30pm - Valencia CF v Real Valladolid
8:30pm - Villarreal FC v RCD Espanyol
11:00pm - Athletic Bilbao v Sevilla FC
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.